• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Serikali ya Uganda haitazalisha umeme zaidi

  (GMT+08:00) 2019-01-29 19:36:38

  Serikali ya Uganda imesema haitatekeleza miradi zaidi ya kuzalisha kawi, na badala yake itatumia fedha kwenye kujenga reli ya kisasa SGR.

  Hata hivyo waziri wa kawi Simon D'Ujanga amesema wawekezaji wa kibinafsi wanaweza kuendeleza mradi wa megawati 840 wa Ayago.

  Amesema ifikapo mwaka 2025 Uganda itakuwa inazalisha umeme kuliko inavyohitaji, na hivyo ni bora kuwekeza kwenye miradi itakayotumia umeme huo.

  Mwishoni mwa mwaka 2018 Uganda ilikuwa inazalisha umeme wa megawati 941 lakini mahiyaji ya juu yalikuwa ni megawati 625.

  Na kwa sasa kuna miradi kadhaa inayoendelea ikiwa ni pamoja na ule wa Isimba (183MW), Karuma (600MW) na Achwa (83MW).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako