• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wakulima wa miwa Busoga wakosa soko

    (GMT+08:00) 2019-01-29 19:42:36

    Wakulima wa miwa katika kanda ndogo ya Busoga nchini Uganda wamesalia na mazao yao kutokana na mahitaji ya chini kutoka kwa wenye viwanda vya sukari.

    Baadhi ya wakulima wanasema miwa imezidi kipindi cha kukomaa kwa miezi 18 na inakauka mashambani.

    Katika kiwanda cha sukari cha Kakira Sugar, karibu na malori 600 yamekuwa yakisubiri nje ya kampuni hiyo lakini bado hawajaruhusiwa kupakua miwa waliowasilisha.

    Msemaji wa chama cha wapanzi wa miwa cha Busoga (BSGA), Godfrey Naitema, aliwahimiza wenye viwanda kuongeza uwezo wao ili kuwalinda wakulima dhidi ya hasara.

    Takwimu kutoka BSGA zinaonyesha kwamba Busoga ina wakulima wa miwa zadi ya 20,000 wenye mashamba makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako