• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waaziri mkuu wa Tanzania aagiza wakulima wa korosho walipwe

    (GMT+08:00) 2019-01-29 19:42:49

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha malipo yote ya fedha za korosho yawe yamelipwa ifikapo Februari 15.

    Aliagiza akaunti za benki 191 za wakulima zilizokuwa na mkanganyiko, taarifa zitolewe kwa wahusika ili waweze kuzirekebisha na wakulima walipwe fedha zao kwa wakati na kuzima malalamiko huku akitaka kuboresha mfumo wa upashanaji habari.

    Agizo hilo la Waziri Mkuu, linafuatilia kauli aliyoitoa Rais John Magufuli hivi karibuni kwamba haelewi kwanini wakulima wa korosho hadi sasa hawajalipwa fedha zao ilhali fedha za malipo hayo zipo.

    Waziri Mkuu Majaliwa aliondoka jana yuko mkoa wa Mtwara kutafuta suluhu ya mkwamo huo kwa kukutana na viongozi wa mikoa inayozalisha zao hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako