• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mjadala kuhusu bomba la mafuta kukamilika Juni

    (GMT+08:00) 2019-01-29 19:43:08

    Serikali za Uganda na Tanzania zimekubaliana kuwa majadiliano yanayohusu utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga yatakamilika ifikapo Juni mwaka huu, ili kuendelea na hatua ya ujenzi wa bomba hilo.

    Hayo yalielezwa jijini Kampala na Waziri wa Nishati wa Tanzania Dk. Medard Kalemani na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni, baada ya kufanyika kikao cha mawaziri wa nchi hizo wanaohusika na mradi huo.

    Dk. Kalemani alisema mradi ulishaanza kutekelezwa kwa kufanyika kazi za awali ikiwamo tathmini ya mazingira ambayo kwa upande wa Tanzania imekamilika na upatikanaji wa eneo kutapojengwa matangi matano yatakayohifadhi mafuta lita 500,000 kila moja mkoani Tanga, ambapo taratibu za ujenzi zinaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako