• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu za pole kwa rais wa Ufilipino kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-01-29 20:08:26

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pole kwa rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Sulu nchini humo.

    Kwenye salamu hizo, rais Xi, kwa niaba ya serikali na wananchi wa China, ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu waliofariki na kuwapa pole majeruhi.

    Pia amesisitiza kuwa China inapinga kithabiti ugaidi wa aina yoyote, ikilaani vikali vitendo vya kigaidi vinavyolenga raia, na China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ikiwemo Ufilipino kupambana kwa pamoja na ugaidi, ili kulinda amani na utulivu wa kimataifa na wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako