• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GOFU: Mashindano ya Gofu Kenya mwaka 2019, yatapata ufadhili zaidi

    (GMT+08:00) 2019-01-30 08:10:35
    Serikali ya Kenya, kupitia wizara ya Utalii na ile ya Michezo, ni miongoni mwa wafadhili watakaoendelea kufadhili zaidi mashindano ya mchezo wa Gofu katika vitengo mbali mbali ya kuwania taji la Kenya Open Golf Championship ya mwaka huu, ambayo yatafanyika katika viwanja vya Karen Country kati ya Machi 14 na 17, jijini Nairobi.

    Mwenyekiti wa shirikisho la gofu nchini humo (KOGL) Peter Kanyago amewashukuru wafadhili hao kwa kuendelea kufadhili mashindano ya mwaka huu na kusema kuwa, kuimarika kwa kiwango cha mchezo huo ndio kulichangia pakubwa kwa wafadhili kujitokeza kufadhili zaidi mashindano ya mchezo wa gofu ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako