SOKA: Ligi kuu ya Uingereza –EPL, vipute kadhaa vilipigwa jana.
(GMT+08:00) 2019-01-30 08:11:41
Ligi kuu ya Uingereza (EPL) iliendelea jana kwa michezo kadhaa kuchezwa nchini humo, Arsenal imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Cardiff City, nao Fulham imeifumua Brighton & Hove Albion goli 4-2, huku Huddersfield Town wamekubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Everton, Wolverhampton Wanderers imeifunga West Ham United kwa magoli 3-0, nayo Manchester United imevutwa shati ya sare ya 2-2 na Burnley, NewCastle United imeibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Manchester City.