• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yawakamata wanachama 54 wa Muslim Brotherhood kwa tuhuma za kupanga vitendo vya kimabavu

    (GMT+08:00) 2019-01-30 08:25:21

    Mamlaka nchini Misri zimewakamata wanachama 54 wa kundi haramu la Muslim Brotherhood kwa tuhuma za kupanga kutekeleza vitendo vya kihasama dhidi ya taasisi za kiserikali, kwenye maadhimisho ya mapinduzi ya Januari 25.

    Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema kupitia taarifa kuwa imepata taarifa kwamba viongozi wa kundi hilo lililoko uhamishoni wamepanga vitendo vya kimabavu dhidi ya nchi, kwa lengo la kuzusha machafuko kwenye kipindi cha maadhimisho ya mapinduzi, yaliyomwondoa madarakani rais wa zamani Hosni Mubarak.

    Taarifa imesema walipanga vitendo vya hujuma kwenye jaribio lao la kueneza vurugu na kuwatisha raia, kwa lengo la kuvuruga usalama na maslahi ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako