• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa Brexit wa Bibi May hatimaye wapata uungaji mkono mkubwa bungeni

    (GMT+08:00) 2019-01-30 08:44:08

    Siku chache baada ya kushindwa vibaya kwenye kura za wabunge katika historia ya Uingereza, hatimaye mpango wa serikali ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya umepata uungaji mkono kwenye bunge la nchi hiyo, kwa kura 317 za ndiyo dhidi ya kura 301 za hapana.

    Ushindi huo wa kura 16 unaipa nguvu serikali ya Uingereza ya kuanza majadiliano mengine na Umoja wa Ulaya kuhusu Brexit.

    Serikali ya Bibi May imeahidi kufanya marekebisho kwenye moja ya mambo yanayofuatiliwa zaidi kwenye suala ya Brexit, yaani suala mpaka wa Ireland Kaskazini, na kupata uungaji mkono kutoka kwa Chama cha Democratic Unionist cha Ireland Kaskazini.

    Kwenye majadiliano hayo Uingereza inatarajia kutofungwa moja kwa moja na Umoja wa Ulaya, na vilevile kutokuwepo kwa mpaka kati ya Jamhuri ya Ireland na Ireland Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako