• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 130 hawajulikani walipo baada ya kuzama kwa mashua mbili pwani mwa Djibouti

    (GMT+08:00) 2019-01-30 08:56:09

    Zaidi ya wahamiaji 130 hawajulikani mahali walipo baada ya mashua mbili kuzama nje ya pwani ya Djibouti.

    Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limetoa taarifa ikisema ajali hii imetokea kwenye eneo la Godoria la sehemu ya Obock kaskazini mashariki mwa Djibouti. Baada ya kupata habari kutoka kwa wakazi wa huko, kikosi cha polisi kilifika kwenye eneo la ajali, na kugundua watu wawili walionusurika na miili ya watu watano.

    Taarifa hiyo inasema kikosi cha ulinzi wa pwani pia kimeshiriki kwenye operesheni za uokoaji, na mashua mbili za doria bado zinaendelea na utafutaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako