• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatarajia kuanzisha Mamlaka ya chakula na dawa

    (GMT+08:00) 2019-01-30 09:42:26

    Kenya itaunda Mamlaka ya chakula na dawa KFDA ili kuongeza hali ya usalama wa chakula nchini humo.

    Katibu mkuu wa wizara ya mifugo ya Kenya Bw. Harry Kimutai amesema, idara hiyo itasaidia kupunguza matukio ya kuwepo kwa kemikali ya aflatoxin katika maziwa na nafaka ambayo imetambuliwa kuwa ni chanzo kikuu cha saratani nchini humo. Pia idara hiyo inatarajia kuhimiza biashara ya ndani na nje ya bidhaa za Kenya.

    Aidha Kenya inatarajia kutoa mpango wa kilimo kuondoa ukosefu wa chakula ndani ya miaka mitano ijayo. Mpango huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa kaya kuwa na akiba ya chakula, na kupunguza idadi ya wakenya waiso na usalama wa chakula kutoka watu milioni 2.7 hadi 0 katika maeneo kame.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako