• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha utoaji wa huduma za utamaduni na utalii wakati wa Sikukuu ya Spring

    (GMT+08:00) 2019-01-30 16:41:04

    Wakati Sikukuu ya Spring inapokaribia, maofisa wa Wizara ya utamaduni na utalii ya China wameelezea hali inayohusu utoaji wa huduma za utamaduni na utalii wakati wa sikukuu hiyo.

    Mwanachama wa kikundi cha uongozaji cha chama cha kikomunisti cha China katika Wizara ya utamaduni na utalii Bw. Wang Xiaofeng ameeleza kuwa, wakati wa sikukuu hiyo, wizara hiyo itatoa huduma mbalimbali za utamaduni na utalii kwa wananchi wote. Anasema:

    "Wizara itazielekeza na kuziunga mkono idara za utamaduni na utalii kwenye sehemu mbalimbali nchini kuandaa maonesho ya urithi wa utamaduni usio wa mali duniani, opera za kienyeji, uchoraji wa mwaka mpya na maonesho ya taa, ili kusherehekea Sikukuu ya Spring. Mbali na hayo pia itafanya shughuli za jadi za utamaduni wakati wa Sikukuu ya Spring, na kuimarisha matangazo ya bidhaa mpya za utalii."

    Katika miaka ya hivi karibuni, kadiri kiwango cha maisha ya wakazi wa mijini na vijijini kinapopanda kwa kasi, ndivyo matumizi ya fedha katika mambo ya utamaduni na utalii yanavyozidi kuongezeka. Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka jana wastani wa matumizi ya fedha katika mambo ya elimu, utamaduni na burudani kote nchini umefikia RMB yuan elfu 2.2, sawa na dola za kimarekani 328, kiasi ambacho kinashika asilimia 11.2 ya wastani wa matumizi ya fedha. Idadi ya watu wanaotalii nchini China imefikia bilioni 5.5 ambayo imeleta pato la utalii yuan trilioni 5.13, sawa na dola za kimarekani bilioni 770, ambalo ni ongezeko la asilimia 10.8 na asilimia 12.3. Idadi ya watu wanaotalii nchi za nje imefikia milioni 141, ambayo imeleta pato la dola za kimarekani bilioni 127.

    Bw. Wang Xiaofeng ameeleza kuwa kutokana na hali hiyo, idadi ya watalii wakati wa Sikukuu ya Spring itaongezeka, na idara husika zitachukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha shughuli za utamaduni na utalii zinaendelea kwa usalama na kwa utaratibu wakati wa sikukuu hiyo. Anasema:

    "Tumeweka mipango kwa pande zote katika usimamizi wa soko inayohusisha mambo ya usalama wa soko, utoaji wa huduma za umma, utoaji wa bidhaa, usimamizi wa soko, matangazo ya habari, kushika zamu wakati wa sikukuu."

    Mbali na hayo shughuli mbalimbali zikiwemo maonesho ya barafu na theluji, vitabu, opera za kienyeji pamoja na wiki ya ubunifu wa bidhaa za utamaduni zitafanyika katika miji 45 ikiwemo Shanghai, Chongqing, Changchun, Hangzhou, Luoyang, Kunming na Urumqi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako