• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ukraine atangaza kushiriki katika uchaguzi ujao wa urais nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-01-30 17:07:41

    Rais Petro Poroschenko wa Ukraine huko Kiev ametangaza kushiriki katika uchaguzi ujao wa urais wa nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya ikulu ya Ukraine, rais Poroschenko ametangaza uamuzi huo katika mkutano kuhusu jinsi Ukraine itakavyoelekea Ulaya uliofanyika huko Kiev. Amesema, amechukua uamuzi huo kutokana na nia yake thabiti ya kulitumikia taifa hilo.

    Rais Poroschenko pia amesema, kama akishinda uchaguzi huo, ataendelea kuhimiza nchi hiyo kujiunga na Jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya, na kuendelea kutimiza ukamilifu wa ardhi ya nchi hiyo kwa njia ya kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako