• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Venezuela akosoa sera ya kidiplomasia ya Marekani

    (GMT+08:00) 2019-01-30 17:07:59

    Rais Nicolas Maduro wa Venezuela katika zoezi la kijeshi lililofanyika jimboni Aragua amekosoa sera ya kidiplomasia ya Marekani na kusema haina msingi.

    Rais Maduro amesema hayo kutokana na kitendo cha msaidizi wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani Bw. John Bolton, wakati akitangaza kuweka vikwazo dhidi ya Venezuela, ambapo daftari aliloshika liliandikiwa 'kutuma askari elfu 5 nchini Colombia'.

    Rais Maduro amesema, kitendo cha Bolton ni vita ya kisaikolojia, na kwamba pamoja na kuwa Venezuela inapitia mapinduzi ya kisiasa yaliyopangwa na Marekani, rais huyo yuko katika mstari wa mbele wa vita, na Venezuela itashinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako