• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa azitaka nchi za Umoja wa Ulaya zisifanye mazungumzo upya na Uingereza kuhusu makubaliano yaliyofikiwa awali

    (GMT+08:00) 2019-01-30 17:10:32

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema nchi za Umoja wa Ulaya zinapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa kutokea hali ngumu baada ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, na hazipaswi kufanya mazungumzo upya kuhusu makubaliano yaliyofikiwa hapo awali kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

    Rais Macron amesema hayo jana kwenye mkutano wa tano wa kilele wa Ulaya Kusini uliofanyika huko Nicosia, mji mkuu wa Cyprus. Ameitaka Uingereza ichukue hatua ili kuepuka kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya bila makubaliano.

    Taarifa iliyotolewa na mkutano wa kilele wa Ulaya Kusini imesema, Umoja wa Ulaya utajitahidi kuifanya Uingereza ijitoe kwenye Umoja huo kwa utaratibu, ili kuhakikisha uthibitisho wa raia na kampuni, vilevile utaharakisha maandalizi ili kukabiliana na changamoto baada ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako