• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zambia asema wasanii wanapaswa kulipwa vizuri kutokana na kazi zao

  (GMT+08:00) 2019-01-30 18:31:41

  Rais Edgar Lungu wa Zambia amewataka watu kuwalipa vizuri wasanii wanapotumia kazi zao.

  Akizungumza na viongozi wa Baraza la Wasanii la Zambia, ikulu hapo jana, rais Lungu amesema Sanaa sio tu sehemu ya burudani lakini pia ni njia ya maisha kwa wasanii, na imekuwa ni sekta kubwa kwenye baadhi ya nchi.

  Rais huyo pia ameeleza kuridhishwa na kazi za wasanii kwa kuwa zinaongeza kipato na kutoa nafasi ya ajira, na kuongeza kuwa ajenda kuu ya serikali ni kuhakikisha ajira na kuongeza kipato kwa wananchi wake, na kwamba sekta yoyote inayochangia ajenda hiyo inatakiwa kuungwa mkono.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako