• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nchi tano zenye silaha halali za nyuklia wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2019-01-30 18:57:14

    Mkutano rasmi wa nchi tano zenye silaha halali za nyuklia umefunguliwa rasmi hapa Beijing, ukiwa ni mkutano rasmi wa kwanza wa nchi hizo kufanyika katika miaka miwili iliyopita.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, wajumbe kutoka nchi hizo tano za China, Marekani, Russia, Uingereza na Ufaransa wamejadiliana kuhusu masuala muhimu ya sekta ya usalama wa kimkakati.

    Kaulimbiu ya mkutano huo ni 'Kuimarisha ushirikiano kati ya nchi tano zenye silaha halali za nyuklia, kulinda mfumo wa makubaliano ya kutoeneza silaha za kinyuklia'. Nchi hizo tano zitafanya mawasiliano ya kina juu ya sera na mikakati ya nyuklia, kujadili ajenda za kupunguza silaha za nyuklia, kutoeneza silaha za nyuklia na kutumia nishati za nyuklia kwa amani.

    Bw. Geng amesema, nchi hizo zimethibitisha wajibu wake maalumu wa kulinda amani, usalama na utulivu wa kimatifa, huku zikitambua kuwa mazingira ya usalama wa kimataifa yanakabiliwa na changamoto kubwa. Nchi hizo tano zinapenda kuimarisha uratibu na kudhibiti migongano, ili kukabiliana na changamoto ya usalama wa kimataifa kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako