• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima watabiri hasara kutokana na mvua

  (GMT+08:00) 2019-01-30 19:12:39

  Wakulima wa tunda aina ya nyanya katika ukanda wa Mlima Kenya nchini Kenya wameonywa kuwa faida kubwa wanayojivunia kwa sasa itasambaratika katika kipindi kifupi kijacho. Wameonywa kuwa msimu wa mvua kubwa ambao unaendelea kwa sasa utakuja na changamoto zake katika kilimo hicho hivyo basi kuadhili vibaya bei katika soko.

  Pia, wameonywa kuwa msimu wa kijibaridi na mvua huandamana na kero la magonjwa ya mimea, hivyo basi kuongeza gharama za uzalishaji ambazo pia humeza pato na hatimaye faida. Akihutubia warsha ya kilimo cha mboga na matunda katika mji wa Maragua ulio katika Kaunti ya Murang'a, afisa wa Usaidizi Kwa Wakulima Nyanjani wa kampuni ya Kemros Seeds, kampuni ambayo hutoa huduma za mbegu, dawa na mbolea kwa Wakulima katika eneo hilo alisema hiyo inafaa kuwa tahathari mwafaka kwa wakati huu. Kwa sasa, bei ya zao hilo imekuwa nzuri kwa soko kwani kilo moja ya nyanya inauzwa kwa Sh64 kwa soko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako