• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jangwa la Sahara laongoza kwa ufisadi

    (GMT+08:00) 2019-01-30 19:14:57

    Jangwa la Sahara Afrika limeorodheshwa kama lililosheheni kwa suala la ufisadi na linazojikokota kupambana nao.

    Kufuatia ripoti ya shirika la kimaifa la kutathmini na kuangazia masuala ya ufisadi duniani, Transparency International iliyotolewa kupitia takwimu zake, CPI, na zinazotolewa kila mwaka, Jangwa hilo limevuta mkia kwa wastani wa asilimia 32 pekee. Linafuatwa kwa karibu na mataifa ya Ulaya Mashariki na Asia ya Kati, kwa wastani wa asilimia 35.

    Katika Jangwa la Sahara nchi ya Somalia kwa mwaka wa saba tena, imekuwa ya mwisho kwa asilimia 10 ikifuatwa na Sudan Kusini asilimia 13.

    Licha ya juhudi za viongozi wa mataifa ya jangwa hilo, kukaza kamba vita dhidi ya ufisadi, siasa na kudorora kwa uchumi, vimetajwa kama vigezo vilivyochangia kwa janga la hili.

    Transparency International pia imesema utawala wa kimabavu na kidikteta katika baadhi ya mataifa hayo pia umelemaza jitihada za kukabili ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako