• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukosefu wa bidhaa za kuuzwa nje chanzo cha kushuka kwa shilingi dhidi ya dola

    (GMT+08:00) 2019-01-30 19:15:19

    Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kutokuwepo kwa bidhaa za kuuzwa nje ya nchi na pia watalii kupungua katika kipindi cha Januari kunaweza kuwa sababu za kushuka kwa shilingi dhidi ya Dola ya Marekani.

    Mkurugenzi wa Uchumi, Utafiti na Sera wa BoT, Suleiman Misango amesema katika kipindi cha miezi ya Desemba na Januari, shilingi hushuka na kupanda kulingana na Dola.

    Kiwango cha ubadilishaji fedha za kigeni cha BoT kimeonyesha kuwa hadi juzi mauzo ya shilingi ya Tanzania yalikuwa Sh2,294 na ilinunuliwa kwa Sh2,271 ikilinganishwa na Sh2,249 na Sh2,227 iliyorekodiwa Januari 29, mwaka jana.

    Ripoti ya soko la fedha ya ya benki hiyo pia imeonyesha kuwa Dola ilikuwa ikibadilishwa kwa wastani wa Sh2,294 kama ilivyorekodiwa Ijumaa wiki iliyopita, kutoka Sh2,249 iliyobadilishwa Januari 29, mwaka uliopita.

    Hata hivyo, Misango alisema kuwa anguko hilo la shilingi linasababishwa na mwezi wa Januari kutokuwa po kwa bidhaa za kuuza nje ya nchi na pia wingi wa watalii.

    Misango alisema mambo yatakuja kubadilika baada ya watalii kuanza kuongezeka nchini humo na uuzwaji wa bidhaa za ndani nje ya nchi, na hivyo wataongeza fedha za kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako