• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Pienaar wa Everton aimwagia sifa Klabu ya Simba, Yawasili Alexandria

    (GMT+08:00) 2019-01-31 08:36:56
    Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton ya Uingereza mwenye asili ya Afrika Kusini Steven Pienaar amewapa ushauri wachezaji wa Afrika kufanya juhudi katika soka na kuangalia kutoka ndani ya bara la Afrika kwa ajili ya kusakata kabumbu nje.

    Kuhusiana na klabu za Simba na Yanga za Tanzania ambazo ndio vilabu vyenye upinzani mkubwa wa jadi na mashabiki wengi Afrika Mashariki, amesema Klabu ya Simba ni maarufu na inasakata kandanda safi zaidi ya Klabu ya Yanga kwa muda mfupi alivyoziona alipokuwa nchini Tanzania kushuhudia michuano ya SportPesa.

    Wakati huo huo, Klabu ya Simba imewasili mjini Alexandria nchini Misri tayari kwa pambano lake dhidi ya wenyeji Al Ahly katika mchezo wa klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako