• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OKA: Matokeo ya Ligi Kuu Uingereza (EPL), The Blues Chali

    (GMT+08:00) 2019-01-31 08:38:49
    Mechi kadhaa za ligi kuu Uingereza (EPL) zilichezwa jana, Chelsea FC aka the Blues hawaamini kwa kile kilichotokea baada ya kukubali kipigo cha goli 4-0 kama wamesimama toka kwa AFC Bournemouth. Nao Tottenham Hotspur wameshinda 2-1 dhidi ya Watford, Southampton wenyewe wametoka sare ya 1-1 dhidi ya Crystal Palace huku Liverpool nao wakitoka sare ya 1-1 na Leicester City.

    Kwingineko: miamba ya soka nchini Ufaransa klabu ya Paris Saint Germain almaarufu kama PSG imethibitisha kuwa mshambuliaji wake raia wa Brazil, Neymar kutokana na kupata majeraha kwenye kifundo cha mguu ule ule ambao aliwahi kuumia kabla ya michuano ya kombe la dunia mwaka jana, atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 10.

    Kuumia kwa nyota huyo sasa atakosa michezo yote miwili dhidi ya miamba ya Uingereza Manchester United na si mechi moja kama ilivyoelezwa awali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako