• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kushirikiana na Benki ya dunia kuvutia uwekezaji binafsi kwenye sekta ya nyumba za bei nafuu

    (GMT+08:00) 2019-01-31 08:56:41

    Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi, miundo mbinu, nyumba na maendeleo ya mijini wa Kenya Bw Charles Mwaura, amesema Kenya inapanga kushirikiana na benki ya dunia kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya nyumba za bei nafuu.

    Bw. Maura amesema kwa sasa Kenya inahitaji dola bilioni 25.7 kutoka sekta ya umma na sekta binafsi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kabla ya mwaka 2022.

    Bw. Mwaura amesema watashirikiana na shirika la uhakikisho wa uwekezaji la benki ya dunia MIGA, kutoa bima ili wawekezaji wa kigeni wawe na imani ya kuwekeza fedha zao kwenye soko la nyumba la Kenya. Amesema serikali haina nia ya kukopa au kuwatwisha mzigo walipa kodi, bali itashirikiana na sekta binafsi kujenga nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako