• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia yasema Tanzania itaendelea kuwa na maendeleo mazuri kwa kuwekeza kwenye elimu ya wasichana

    (GMT+08:00) 2019-01-31 08:57:04

    Ripoti iliyotolewa na benki ya dunia imesema kuwaelimisha wasichana na kukomesha ndoa za utotoni kumetajwa kuwa kutachochea maendeleo na kupunguza umaskini nchini Tanzania.

    Ripoti hiyo imesema kama wasichana hawataelimishwa wataishia kuwa na mishahara midogo, kuwa kwenye hatari kubwa za kiafya, kuwa kwenye hatari ya kuwa wahanga wa kupigwa na waume wao, ongezeko kubwa la watu na kuathiriwa na umaskini.

    Ripoti hiyo imesema mmoja kati ya wasichana watatu nchini Tanzania anaolewa akiwa chini ya umri wa miaka 18, na mmoja kati ya wasichana wanne anapata mtoto chini ya umri wa miaka 18. Hali hii imechangia sana kuwa na wasichana wachache wanaomaliza elimu ya sekondari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako