• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yamshtaki aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Somali kwa kuzusha mgogoro wa ndani

    (GMT+08:00) 2019-01-31 09:17:47

    Mwanasheria mkuu wa Ethiopia amemshtaki Abdi Mohammed Omer aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Somali mashariki mwa nchi hiyo kwa makosa ya jinai ya kuzusha mgogoro wa ndani.

    Bw. Omer ameshtakiwa kuunda kundi la vijana la Heego, na kuwaamuru kuwashambulia kikatili wakazi wasio wa kabila la Wasomali wa mkoa huo katika vurugu zilizoendelea kwa siku kadhaa mwezi Agosti mwaka jana.

    Mwanasharia huyo pia amewashtaki watu wengine 46 wanaotuhumiwa kuwashambulia watu wasio wa kabila la Wasomali.

    Vurugu zilizotokea mwezi Agosti mwaka jana huko Jijiga mji mkuu wa mkoa wa Somali na miji mingine midogo ya mkoa huo, zilisababisha vifo vya watu 58, na wengine 266 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako