• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru mpya ya Mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yafunguliwa Washington

    (GMT+08:00) 2019-01-31 09:28:19

    China na Marekani zimeanza duru mpya ya mazungumzo ya ngazi ya juu ili kutatua mgongano wa kiuchumi na kibishara kati ya nchi hizo mbili.

    Mazungumzo hayo ya siku mbili yanaashiria kuwa mafanikio yamepatikana kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Donald Trump mjini Buenos Aires, Argentina mwezi uliopita. Viongozi wa nchi mbili wanaona pande zote mbili zinapaswa kufikia makubaliano ya kunufaishana ndani ya siku 90, ili kumaliza mgongano wa kibiashara wa kutozana ushuru mkubwa kwenye sekta ya uagizaji kutoka nje, ambayo yameendelea kwa miezi mingi.

    Mazungumzo hayo yanatarajiwa kumaliza leo alasiri. Ikulu ya Marekani imesema rais Donald Trump leo atakutana na kiongozi wa ujumbe wa China, naibu waziri mkuu wa China Bw Liu He.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako