• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juncker asema Umoja wa Ulaya hautafanya tena mjadala na Uingereza juu ya makubaliano ya Brexit

    (GMT+08:00) 2019-01-31 16:30:25

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean Juncker amejibu juu ya matakwa ya bunge la Uingereza kuhusu kurekebisha makubaliano ya Brexit, na kusema, Umoja huo hautafanya mjadala mpya na Uingereza juu ya makubaliano ya Brexit.

    Akizungumza kwenye Bunge la Ulaya, Bw. Juncker amesema, makubaliano ya Brexit yaliyofikiwa awali na Umoja wa Ulaya na Uingereza ni mpango mzuri zaidi na wa kipekee wa Uingereza kujitoa kutoka Umoja huo, na matokeo ya upigaji kura wa baraza la chini la bunge la Uingereza hayatabadilisha msimamo huo.

    Bw. Juncker amesema, pande hizo mbili zimeeleza kidhahiri kwa mara nyingi msimamo wa kutoweka mpaka mgumu katika kisiwa cha Ireland, na kusema ili kuepusha kurudia makosa ya kihistoria, inapaswa kuweka mpango mwingine kama uhakikisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako