• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa televisheni za satelaiti unaolenga kuwanufaisha wanavijiji barani Afrika waingia katika kipindi cha mwisho nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-01-31 18:08:49

    Wakati wa Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2015, rais Xi Jinping wa China alitangaza mradi wa televisheni za satelaiti unaolenga kunufaisha vijiji elfu 10 katika nchi 25 barani Afrika. Mradi unaotekelezwa na Kampuni ya Startimes ya China umeanza kutekelezwa katika nchi nyingi barani Afrika zikiwemo Msumbiji, Zambia, Kongo Brazzaville, Uganda na Kenya, na mradi unaoendelea nchini Kenya umeingia katika kipindi cha mwisho.

    Ili kuitikia mipango ya ushirikiano iliyotolewa na rais Xi wa China katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, mradi huo wa televisheni za satelaiti umeanza kutekelezwa rasmi kuanzia mwezi Juni mwaka 2018. Mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 84.27 utahusisha vijiji 800 kwenye kaunti 47 nchini Kenya. Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia wa Kenya Bw. Joe Mucheru alisema kwenye sherehe ya uzinduzi wa shughuli hizo:

    " Mradi huu si kama tu utasaidia televisheni za kidijitali kuenea kote nchini Kenya, bali pia utahimiza mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Kenya. Kuanzishwa kwa mradi huo kunaonesha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili unazidi kuimarishwa na kutafuta kwa pamoja maendeleo ya kiuchumi na kisiasa."

    Baada ya juhudi za nusu mwaka kati ya pande zote mbili za China na Kenya, mradi huo umetekelezwa kwa pande zote na kuingia katika kipindi cha mwisho. Mwanakijiji wa kijiji cha Uthiru Bw. Michael Ng'ang'a amesema zamani familia yake haikupata ishara ya televisheni, watoto wake walikuwa wakitaka kutazama televisheni wanapaswa kwenda kwa wajirani. Lakini sasa kutokana na mradi huo, wanaweza kutazama televisheni ama vipindi vya kichina ama vya kienyeji, hali ambayo inawafurahisha sana.

    Takwimu zimeonesha kuwa, jumla ya familia zaidi ya 16,000 na mashirika 2,400 ya umma yamenufaika na mradi huo. Kampuni ya Startimes nchini Kenya pia imewaandaa wafanyakazi kwa ajili ya kila kijiji, na idadi ya wafanyakazi imefikia 1,600. Bw. Peter anashughulikia utoaji wa huduma kwenye kijiji cha Uthiru amesema, wafundi wa kampuni ya Startimes wamemfundisha ujuzi unaohitajika wakati wa kutengeneza mitambo. Sasa yeye binafsi amejulikana kutokana na mradi huo, kwani wanakijiji wote wanajua amepewa mafunzo yanayoandaliwa na kampuni ya China, na kila wanapokumbwa na matatizo wanakwenda kwake. Mradi huo umesaidia kuongeza uwezo wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako