• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya boti nchini Djibouti yafikia 52

  (GMT+08:00) 2019-01-31 18:17:35

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema idadi ya watu waliofariki baada ya boti mbili zilizobeba wahamiaji kuzama kwenye pwani ya Djibouti imefikia 52.

  Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, watu 16 wameokolewa katika ajali hiyo iliyotokea Obock, katika pwani ya Bahari Nyekundu nchini Djibouti.

  Ajali hii inasemekana kuwa moja ya ajali nyingi zinazotokea kwenye pwani hiyo, kutokana na wahamiaji kutoka Afrika Mashariki wakijitahidi kuvuka kwenye njia hiyo ya hatari kwenye Mashariki ya Kati kupitia Yemen kwa lengo la kutafuta maisha mazuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako