• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan asema maana pekee ya uchaguzi ni kubadili serikali

    (GMT+08:00) 2019-01-31 18:52:04

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesema serikali na rais wanaweza kubadilishwa tu kwa kupitia upigaji wa kura.

    Akizungumza na wafuasi wake katika mkoa wa Kassala, mashariki mwa Sudan hii leo, rais Bashir amesema kubadili serikali na rais wake hakuwezi kufanyika kupitia mitandao ya kijamii, bali kwa kupiga kura. Rais Bashir amekiri kuwa Sudan inapitia wakati mgumu, na kwamba serikali yake inafanya juhudi kukabiliana na changamoto hiyo. Pia amerejea tena ahadi yake ya kufanya majadiliano na vijana ili kusikia sauti yao, kwa kuwa ni uhakikisho wa Sudan ya baadaye.

    Wakati huohuo, rais Bashir ameamua kufungua tena mpaka kati ya nchi yake na nchi jirani ya Eritrea. Amesema siasa inaweza kuwatenganisha, lakini kinachowakutanisha pamoja ni kikubwa kuliko kinachowatenganisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako