• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia imeongeza mara tatu ukubwa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole

  (GMT+08:00) 2019-01-31 18:56:27

  Jiji kuu la Ethiopia linalenga kuimarisha nafasi yake kama kituo cha ndege kinachoongoza kwa kupanua uwanja wa ndege na kuongeza mara tatu uwezo wa kuhudumia abiria.

  Mwaka jana Addis Ababa iliipiku Dubai kama kituo kinachoongoza cha ubadilishaji wa ndege kwa safari za nchi zliizoko chini ya jangwa la sahara.

  Tarehe 27 Januari,Waziri Mkuu wa Ethipoia,Abiy Ahmed alizindua eneo jipya la abiria lililofanyiwa upanuzi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole,kituo kikuu cha ndege za Shirika la Ethiopia mjini Addis Ababa.

  Mradi huo ambao ulifadhiliwa na kujengwa na China kwa gharama ya $363 milioni, umeongeza mara tatu ukubwa wa uwaja huo wa ndege na hivi sasa unaweza kuhudumia abiria milioni 22 kwa mwaka kutoka uwezo wake wa sasa wa abiria milioni 7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako