• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa korosho Tanzania wapata mnunuzi mkubwa kutoka Kenya.

    (GMT+08:00) 2019-01-31 19:00:02

    Kampuni ya Indopower Solutions ya Kenya jana ilitia saini ya makubaliano ya ununuzi wa tani 100,000 za korosho kwa Tsh.bilioni 418 ,fedha ambazo zitalipwa ndani ya siku saba kuanzia jana.

    Mkataba wa mauziano ulitiwa saini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Makao Makuu ya Jumiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ,Hussein Mansoor na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Indopower Solutions,Brian Mutembei.

    Hafla hiyo ilishuhudiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi,Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda,Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa,Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof Florens Luoga,makatibu wa Wizara hizo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako