• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na Emir wa Qatar

    (GMT+08:00) 2019-01-31 20:17:46
    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani ambaye yupo ziara nchini China.

    Viongozi hao wamekubali kwa kauli moja kukuza kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kupata maendeleo kwa pamoja.

    Rais Xi amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinatakiwa kuoanisha mikakati ya maendeleo na kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuimarisha mawasiliano katika kupambana na ugaidi wa kimataifa na siasa kali, kuzidi kuimarisha mawasiliano ya utamaduni, kuhimiza ushirikiano wa utalii, utamaduni, michezo na vyombo vya habari.

    Naye Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amesifu msimamo wa kiujenzi wa China katika mambo ya pande nyingi pamoja na masuala ya mashariki ya kati na sehemu ya Ghuba, pia inapenda kushirikiana kuimarisha mawasiliano na uratibu, na kukuza ushirikiano na China katika mapambano dhidi ya ugaidi na siasa kali.

    Viongozi hao pia wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Rais Xi pia amekutana na mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Bw. Thomas Bach, akisisitiza kuwa China itaiandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi isiyo na uchafuzi wa mazingira, ya kunufaishana, yenye uwazi, na isiyo na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako