• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaidhinisha ujenzi wa kituo cha kupambana na milipuko

    (GMT+08:00) 2019-02-01 08:27:28

    Baraza la mawaziri la Kenya limeidhinisha kuanzishwa kwa kituo cha kupambana na milipuko mjini Nairobi, ili kusaidia mapambano dhidi ya ugaidi nchini humo.

    Mkutano wa baraza hilo ulioongozwa na rais Uhuru Kenyatta, umesema Ujerumani imetoa dola za kimarekeni milioni 2.07 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupambana na mabomu ya kienyeji mjini Nairobi.

    Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema kituo hicho kitafanya kazi muhimu hasa katika kipindi ambacho jeshi la Kenya litaendelea kuwepo nchini Somalia, ambako mabomu ya kienyeji yanatumiwa mara kwa mara na kundi la Al-Shabaab.

    Polisi nchini Kenya wamesema wapiganaji wa Al-Shabaab wamebadilisha mkakati wao na kuanza kutumia mabomu ya kienyeji katika kufanya mashambulizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako