• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia amtaka mkuu mpya wa AMISOM kuendeleza mapambano dhidi ya Al Shabaab

    (GMT+08:00) 2019-02-01 08:42:46

    Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw. Francisco Madeira amemtaka kamanda mpya wa vikosi vya tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM Bw. Tigabu Wondimhunegn kuendelea na mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab nchini Somalia.

    Bw. Madeira amesema bado kuna kazi kubwa inayotakiwa kufanyika, na idhini ya uwepo wa vikosi hivyo nchini Somalia bado ipo. Amesema licha ya kuwa kuna kazi kubwa, anaamini kuwa kamanda mpya anaweza kukamilisha kazi.

    Habari nyingine kutoka Somalia zinasema jeshi la Marekani limefanya shambulizi karibu na kambi moja ya magaidi katikati ya Somalia, na kuwaua magaidi 24 wa kundi la Al-Shabaab. Mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani amesema shambulizi hilo ni sehemu ya juhudi za kulisaidia jeshi la Somalia kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako