• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu Bingwa Afrika-Aussem alia na baridi, atumia video mazoezini

    (GMT+08:00) 2019-02-01 08:58:44
    Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems ameelezea kuhusiana na programu ya mazoezi ya siku ya kwanza baada ya kuwasili nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

    Aussems amesema, baridi ndilo jambo lililowapa changamoto lakini kwa siku watakazokuwepo, watazoea na kuwa fiti kwa mchezo huo. Simba inatarajia kupambana na wenyeji Al Ahly katika mchezo wa kundi D kesho Jumamosi, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria Misri.

    Wakati hayo yakiendelea, wekundu hao wa Mismbazi wameweka wazi kuwa dili la kumtoa mshambuliaji wake mahiri Ramadhani Kichuya kwa mkopo kwa klabu ya Pharco limekamilika. Kichuya amesaini mkataba wa miaka 4 na klabu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako