• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Nyota wa Manchester United akubali kujiunga na klabu ya China

    (GMT+08:00) 2019-02-01 08:59:58
    Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini ameridhia makubaliano ya mkataba binafsi na klabu ya Shandong Luneng kwa lengo la kuhamia klabu hiyo ya China.

    United wamekataa kutoa tamko lolote ikiwa malipo yoyote yamefikiwa kumnunua mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye alitia saini nao mwaka 2018.

    Fellaini mwenye umri wa miaka 31, alikuwa mchezaji mkubwa wa kwanza aliyesainiwa baada ya enzi ya Sir Alex Ferguson, akijiunga na Manchester Utd kwa kiasi cha pauni milioni 27.5 mwaka 2013 akitokea Everton.

    Mwisho wa dirisha la uhamisho wa wachezaji katika ligi ya China ni Februari 28.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako