• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malori yaliyobeba pembe za ndovu na magamba ya kakakuona yakamatwa Uganda

    (GMT+08:00) 2019-02-01 09:10:36

    Mamlaka ya kodi ya Uganda imekamata malori matatu yaliyobeba pembe za ndovu na magamba ya kakakuona kwenye kivuko cha mpakani cha Elegu kati ya Uganda na Sudan Kusini.

    Msemaji wa mamlaka hiyo Bw. Vincent Suruma amesema vitu hivi vinatoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na vimepitia Sudan Kusini na kufikishwa Uganda.

    Bw. Vincent amesema wavietnam wawili wamekamatwa pamoja na malori hayo, walificha pembe za ndovu na magamba ya kakakuona ndani ya mbao zilizopasuliwa, na kuzifunga kwa nta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako