• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yaeleza wasiwasi juu ya vitendo vya kukiuka makubaliano ya amani vinavyoendelea Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-02-01 09:10:56

    Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imeeleza kusikitishwa na vitendo vinavyoendelea vya ukiukaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka jana na pande zinazopambana.

    Mjumbe maalumu wa IGAD anayeshughulikia suala la Sudan Kusini Bw. Ismail Wais amesema baada ya kuathiriwa na vita kwa zaidi ya miaka mitano, watu wa Sudan Kusini wanatumai kujenga upya maisha yao, na vitendo vya kukiuka makubaliano ya amani havikubaliki.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na tume ya kuchunguza utekelezaji wa makubaliano ya amani RJMEC nchini Sudan Kusini, serikali na makundi ya waasi wote wanapanga majeshi katika sehemu ya Yei kusini mwa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako