Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif amepongeza kuanzishwa kwa njia mpya ya malipo na nchi tatu za Ulaya Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, ambazo zitasaidia makampuni ya nchi hizo kuendelea kufanya biashara na Iran.
Bw. Zarif amesema, Iran iko tayari kuendelea kuwasiliana na nchi za Ulaya kwenye msingi wa kuheshimiana. Mapema siku hiyo Umoja wa Ulaya umetangaza kuanzisha shirika jipya la INSTEX kulinda biashara na Iran, ili kuepuka vikwazo vya Marekani, baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya suala la nyuklia la Iran JCPOA.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |