• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kuvumilia maendeleo ya sayansi na teknolojia ya nchi nyingine

    (GMT+08:00) 2019-02-01 09:49:58

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inataka Marekani iwe na msimamo wa kufungua mlango na kuvumilia kuhusu maendeleo ya sayansi na teknolojia ya nchi nyingine.

    Bw. Geng ameyasema hayo alipoulizwa swali kuhusu mbunge wa Marekani kuonyesha wasiwasi kwa mashirika makubwa ya kitaifa ya teknolojia ya China, na kusema China inataka kuchukua nafasi ya uongozi ya Marekani katika sayansi na teknolojia. Amesema China inakubali Marekani ni nchi yenye nguvu kubwa zaidi kisayansi na teknolojia, lakini haifai kuzuia maendeleo ya nchi nyingine.

    Habari nyingine zinasema, Shirika la Haki Miliki za ubunifu la Umoja wa Mataifa jana lilitoa ripoti ikisema, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ustawi wa soko la bidhaa za akili bandia duniani, uvumbuzi wa teknolojia ya akili bandia umetolewa kwa wingi, na China na Marekani zimeshika nafasi za mbele kwa maendeleo ya teknolojia hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako