• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani yamalizika

    (GMT+08:00) 2019-02-01 10:21:06

    Mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani yamemalizika mjini Washington.

    Ujumbe wa China ulioongozwa na naibu waziri mkuu Bw. Liu He na ujumbe wa Marekani ulioongozwa na mwakilishi wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer, umefanya majadiliano mahususi, ya dhati, na ya kiujenzi kuhusu mada wanazofuatilia kwa pamoja, ikiwemo uwiano wa biashara, usafirishaji wa teknolojia, ulinzi wa haki miliki za ubunifu, vizuizi visivyo vya ushuru, huduma, kilimo na mfumo wa utekelezaji. Pia pande hizo mbili zimepanga utaratibu wa majadiliano yajayo na ratiba.

    China na Marekani zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kulinda haki miliki za ubunifu na usafirishaji wa teknolojia, na kwamba kuandaa mazingira ya soko lenye ushindani wa usawa kunaendana na sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China. Pia China itapanua uagizaji wa bidhaa za kilimo, nishati, za kiviwanda na huduma kutoka Marekani kwa lengo la kuhudumia maendeleo ya uchumi wa China na mahitaji ya wananchi kwa maisha bora.

    Baada ya mazungumzo hayo, naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He alikutana na rais Donald Trump. Rais Trump amesema raundi hiyo ya mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na China imepata maendeleo muhimu, na anatarajia kuwa pande hizo zitafikia makubaliano mazuri mapema iwezekanavyo, ambayo ni muhimu kwa nchi hizo mbili na dunia nzima. Ameeleza kuwa mwakilishi wa biashara wa Marekani Robert Lighthizer na waziri wa fedha Steven Mnuchin katikati ya mwezi Februari wataongoza ujumbe wa Marekani kuja China kuendelea na mazungumzo hayo, na kwamba anatarajia kukutana na rais Xi Jinping wa China mapema na kushuhudia kwa pamoja wakati wa kihistoria wa kufikiwa kwa makubaliano ya kibiashara kati ya Marekani na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako