• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanahabari wa Misri waona uzoefu wa China ni njia nzuri ya kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2019-02-01 10:59:58

    Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Misri wanaona kuwa, uzoefu wa China ambao unazingatia kupambana na vitendo halisi vya kigaidi na kung'oa mzizi wa ugaidi ni njia nzuri ya kupambana na ugaidi katika zama mpya.

    Ujumbe wa waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Misri vikiwemo gazeti la Al-Ahram, gazeti la Algomhuria na Televisheni ya Mto Nile umetembelea mkoa wa Xinjiang, China kuanzia tarehe 25 hadi 31 mwezi uliopita. Wanahabari hao walijionea maisha ya wakazi wa mijini na vijijini, na kutembelea vituo vya kutoa mafunzo ya ustadi kazi mkoani humo.

    Baada ya kutembelea kiwanda cha nguo cha tarafa ya Baren, Bw. Abdelhalim Ahmed Ali kutoka gazeti la Algomhuria amesema nchini Misri, inawabidi wakulima kwenda mijini ili kupata kazi za viwandani, lakini wakulima wa Xinjiang wanaweza kujiondoa kwenye umaskini.

    Bw. Yunus Gaballa Aly Kamal wa gazeti la Al-Ahram alitembelea kituo cha mafunzo ya ajira, alisema kituo hicho si kama kilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya magharibi, kinawafundisha wanafunzi uwezo wa ajira, mambo ya sheria na kuwaambia kuwa na tabia nzuri ya kuwatendea watu wengine, na hii ni mbinu nzuri ya kutokomeza itikadi kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako