• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Marekani yazindua njia mpya ya kutatua suala katika mazungumzo yao ya biashara

  (GMT+08:00) 2019-02-01 12:19:34

  Mazungumzo ya ngazi ya juu ya biashara kati ya China na Marekani yalimalizika Alhamisi mjini Washington. Kwa siku mbili, chini ya maelekezo ya makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, pande hizo zimefanya majadiliano mahususi, ya dhati, na ya kiujenzi kuhusu mada zinazofuatilia kwa pamoja, ikiwemo uwiano wa biashara, usafirishaji wa teknolojia, ulinzi wa haki miliki za ubunifu, vizuizi visivyo vya ushuru, huduma, kilimo na mfumo wa utekelezaji. Pia pande hizo mbili zimepanga utaratibu wa majadiliano yajayo na ratiba.

  Si rahisi kupatikana kwa matokeo hayo, lakini pia ni kama ilivyotarajiwa. Kutoka ikulu ya Marekani kuukabirisha ujio wa ujumbe wa China katika taarifa yake hadi rais Donald Trump kukutana na naibu waziri mkuu Bw. Liu He aliyeongoza ujumbe wa China baada ya mazungumzo hayo, na kueleza kuwa ujumbe wa Marekani utakuja China katikati ya mwezi Februari na kuendelea na mazungumzo hayo, na matumaini yake ya kukutana na rais Xi Jinping wa China, mambo hayo yote yameashiria kuwa Marekani pia inataka kuona matokeo mazuri. Katika raundi hii ya mazungumzo, China na Marekani zimeeleza ufuatiliaji wao kwa udhati, na kujitahidi kutafuta maslahi ya pamoja kuhusu mada moja baada ya nyingine, ndiyo maana zimepata maendeleo muhimu kwa kipindi cha sasa yanayoonesha kanuni za kusaidiana na mafanikio kwa pamoja.

  Katika miaka 40 iliyopita tangu sera ya mageuzi na ufunguaji malngo ianzwe kutekelezwa, ni kwa sababu China inaelewa kwa usahihi uhusiano kati ya "changamoto" na "fursa", inaweza kuongeza uwezo wa kukabiliana na hatari na kiwango cha maendeleo. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa safari hii, China itapanua uagizaji wa bidhaa za kilimo, nishati, za kiviwanda na huduma kutoka Marekani, kitendo ambacho kwa kweli kinaweza kuhudumia maendeleo ya uchumi wa China na mahitaji ya wananchi kwa maisha bora.

  China itaendelea kuimarisha mageuzi na ufunguaji mlango bila kujali kuwepo au la kwa mikwaruzano ya kibiashara kati yake na Marekani, lakini hali halisi ni kuwa baadhi ya madai yaliyotolewa na Marekani yanaendeana na mwelekeo wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China, na kujibu madai hayo kunaweza kuhimiza maendeleo mazuri ya uchumi wa China. Mtazamo huo ni mbinu ya China ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya kimataifa, pia ni njia mpya iliyozinduliwa katika kutatua suala kwenye mazungumzo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako