• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zajenga mfumo maalumu ili kuendelea kufanya biashara na Iran

    (GMT+08:00) 2019-02-01 16:38:06

    Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema, nchi hiyo pamoja na Ujerumani na Uingereza zimeanzisha mfumo maalumu wa kufanya biashara na Iran, ambayo ni hatua muhimu inayochukuliwa na nchi za Ulaya kuendelea kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran baada ya Marekani kujitoa kutoka makubaliano hayo.

    Vyombo vya habari nchini humo vimesema, mfumo huu maalumu ni wa malipo nje ya mfumo wa kifedha wa ulimwengu unaoongozwa na Marekani, ambao unaweza kuufanya Umoja wa Ulaya kuendelea kufanya biashara na Iran na kuyasaidia mashirika ya Ulaya kukwepa vikwazo vya upande mmoja vinavyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.

    Mfumo huo umeonesha nia thabiti na juhudi za kudumu za nchi hizo tatu kuendelea kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran, lakini zimesema utekelezaji wa pande zote wa makubaliano hayo wa Iran ni msingi wa utekelezaji wa mfumo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako