• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande zote husika zitafute ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-02-01 18:13:59

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inazitaka pande zote husika zitafute ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Venezuela kwa njia ya mazungumzo, na kwamba China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kufanya juhudi za pamoja katika hatua hiyo.

    Bw. Geng Shuang pia amesisitiza kuwa China itafuata kanuni ya kunufaishana kwa usawa, kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja ili kuhimiza mawasiliano na ushirikiano na Venezuela katika sekta mbalimbali.

    Geng Shuang pia ametoa salamu za Sikukuu ya Spring kwa marafiki wote wanaofuatilia mambo ya kidiplomasia ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako