• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa yakubali kuisaidia Zambia kujenga kituo cha utalii ili kuboresha sanaa na utamaduni

    (GMT+08:00) 2019-02-01 18:22:30

    Ufaransa imeahidi kuisaidia Zambia kujenga kituo kikubwa cha utalii ili nchi hiyo iweze kutangaza zaidi utalii na sanaa na utamaduni.

    Balozi wa Ufaransa nchini Zambia Sylvain Berger ametoa ahadi hiyo alipokutana na waziri wa utalii na sanaa wa Zambia, Charles Banda. Balozi Berger amesema nchi yake inafurahia uhusiano na Zambia uliodumu kwa miaka 55, na kwamba nchi hizo mbili zimefanya kazi kwa karibu katika maeneo ya mendeleo ya uchumi.

    Kwa upande wake, Bw. Banda ameishukuru Ufaransa kwa kuisaidia nchi yake kujenga kituo hicho, akisema kitasaidia kuongeza umaarufu wa utamaduni na sanaa. Pia amesema wizara yake itafanya juhudi zote kuhakikisha kituo hicho kinajengwa kwenye eneo la katikati, na pia kitatumika kama kituo cha sanaa na utamaduni na shughuli nyingine zinazohusiana na utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako