• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar yaonya dhidi ya kuongeza vyanzo vya mapato

    (GMT+08:00) 2019-02-01 18:43:43

    Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt Khalid Salum Mohamed amewataka watendaji wa serikali kuachana na tabia ya kuwaongezea wananchi mzigo kwa kuongeza vyanzo vya mapato.

    Aliyasema hayo kwenye kikao cha kuibua mambo ya kuzingatia katika utayarishaji bajeti kwa mwaka 2019/20 kilichowashirikisha watendaji wakuu wa Serikali, serikali za mitaa na taasisi zinazohusiana na ukuaji wa uchumi.

    Dkt Khalid alisema lengo la kikao hicho ni utekelezaji wa sheria namba 12 ya mwaka 2016 ambayo inataka kuanzishwa kwa jukwaa la bajeti na uchumi.

    Alisema miongoni mwa maeneo yanayohitajika kupitiwa upya ni hali ya uchumi; mfumo wa mapato; vyanzo vya mapato vinavyofanya kazi; matumizi ya fedha na changamoto zilizopo.

    Pia, alisema kutakuwa na utaratibu wa kuangalia sekta tatu zilizogatuliwa ikiwamo elimu, afya na kilimo ili kuhakikisha kunakuwa na urahisi wa upelekaji huduma za jamii na kufikia malengo ya Serikali.

    Eneo jingine ni uhaulishaji fedha kwa taasisi zilizogatuiliwa, ambao unapaswa kufanywa kwa kuzingatia vigezo ikiwamo idadi ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako