• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa mifugo Kenya kupata huduma za AI

  (GMT+08:00) 2019-02-01 18:45:45

  Gavana Ferdinand Waititu amesema kila mfugaji wa ng'ombe wa maziwa Kiambu atapata huduma za uhamilishaji (AI) bila malipo. Waititu amesema mpango huu unalenga kuimarisha uzalishaji wa maziwa katika kaunti hiyo.

  Ameongeza kuwa mpango huo utagharimu zaidi ya Sh30 milioni, na tayari pikipiki zitakazosafirisha wataalamu wa huduma hii zimetolewa.

  AI ni njia bora ya uzalishaji wa teknolojia inayoboresha mifugo. Kiambu ni mojawapo ya kaunti zenye kampuni tajika za maziwa nchini Kenya kama Brookside na Githunguri, pamoja na wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kisasa.

  Hii inakuja miezi michache tu baada ya Gavana wa Kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja kutangaza kuwa kila mfugaji wa ng'ombe wa maziwa atakuwa akipata huduma za AI kwa Sh500 kila ng'ombe.

  Samboja alisema hilo lililenga kuimarisha sekta ya ufugaji, hasa uzalishaji wa maziwa. Mwaka wa 2016, Nyeri pia ilianza kutoa huduma hizi kwa bei nafuu. Gharama ya huduma hii nchini huwa kati ya Sh1,000-Sh4,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako