• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi 34 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wauawa kazini mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2019-02-01 21:07:52

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, mwaka 2018 wafanyakazi 34 wa Umoja wa Mataifa waliuawa kazini kwenye mashambulizi, na idadi hiyo ni ndogo zaidi katika miaka 5 iliyopita.

    Bw. Dujarric amenukuu ripoti iliyotolewa na Shirikisho la Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuwa, watu hao 34 ni pamoja na askari 26 wa kulinda amani na watumishi wanane. Kati ya askari waliouawa, 11 walikuwa kwenye kikosi cha kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, wanane walikuwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na wengine 7 kutoka kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Afrika ya Kati.

    Shirikisho la wafanykazi wa Umoja wa Mataifa limeutaka Umoja huo na nchi wanachama wake utoe uungaji mkono wa lazima kwa wafanyakazi wa Umoja huo, pia kuwakamata wahalifu waliowashambulia wafanyakazi hao kwa mujibu wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako